SI KWELI Tangazo la fursa za masomo nchini Norway 2022/2023

SI KWELI Tangazo la fursa za masomo nchini Norway 2022/2023

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Kwenye matangazo yao yanayoonekana mtandaoni wanaonesha ufadhili wa Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway, huku maelezo yakieleza chuo kinachohusika na scholaships hizo kuwa ni Chuo Kikuu cha Bergen.

Suala hilo linaleta mkanganyiko na kuondoa kabisa imani na tangazo hilo kwani vyuo hivyo vinabeba majina ya miji miwili tofauti nchini humo. Oslo ni mji mkuu wa Norway, na Bergen ni jiji la pili kwa ukubwa na kuna umbali wa takribani kilomita 460 kati ya miji hiyo miwili.

Pia inatia mashaka kwamba ufadhili wa masomo halali ungetangazwa kwenye tovuti iliyoundwa vibaya na maandishi yaliyoandikwa vibaya. Hivyo, inatia shaka kuwa tangazo hilo limetolewa na taasisi ya elimu ya juu.

Suala lingine ni kuwa ukibofya manenoAPPLY NOWhata bila kujaza taarifa zozote tovuti hiyo inaleta ujumbe wa kupongeza kuwa maombi yametumwa. Hili ni jambo lingine la kutilia shaka.

Hata hivyo, tovuti hiyo haitoi kiunganishi chochote cha tovuti za Chuo Kikuu cha Oslo na Chuo Kikuu cha Bergen. Hii ni dalili kwamba hakuna uhusiano wa kweli na vyuo vikuu hivi au udhamini wowote unaotolewa nao.
Back
Top Bottom