<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- Februari 1, 2023, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu A. Lissu aliweka picha nne kwenye Mtandao wa Twitter zikiambatana na ujumbe unaosema “Reconnecting with Chairman Mbowe after years of enforced separation” baada ya kutokuwa pamoja tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Ukizitazama picha hizi halisi, hakuna hata moja yenye Chupa ya konyagi kama baadhi ya watu wanavyodai.
Hivyo, kwa kutumia ushahidi huu, picha yenye Chupa ya Konyagi siyo halisi na haina ukweli wowote.
Chupa ya konyagi inayoonekana kwenye picha ni istizahi inayofanywa na wapinzani wa Mbowe ambao wanaamini maneno yaliyosemwa Bungeni miaka kadhaa iliyopita kuwa tukio la yeye kuanguka kwenye ngazi lilisababishwa na ulevi wa konyagi.