SI KWELI Nywele na kucha za mtu huendelea kukua hata baada ya kufariki

SI KWELI Nywele na kucha za mtu huendelea kukua hata baada ya kufariki

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Ngozi na kucha huwa haziendelei kukua baada ya kupatwa na umauti. Hata hivyo, ni muhimu kukubaliana na ukweli kuwa sehemu hizi huonekana zikiwa zinaongezeka urefu tofauti na zilivyokuwa awali.

Mwili hupoteza kiasi kikubwa cha maji baada ya kifo (dehydration), hivyo ngozi huanza kusinyaa na kujivuta (shrinking).

Kusinyaa na kujivuta huku kwa ngozi hufanya kiasi fulani cha kucha na nywele zilizokuwa zimeshikizwa chini yake zijivute kwa nje, hivyo kuonekana zikiwa zimeongezeka urefu kwa kiasi fulani. Huu siyo ukuaji, bali ni ongezeko la urefu linalotokana na kusinyaa kwa ngozi.

Aidha, ukuaji wa kucha na nywele za mwili huhitaji nishati inayozalishwa na glucose ambayo huwa haipo kwa wakati huo.

Pia, kwa mujibu wa Jarida la kitabibu la The BMJ, mfumo unaoratibu ukuaji wa sehemu hizi kupitia vichocheo vya mwili (homoni) husimama baada ya kifo, hivyo hakuna namna yoyote inayoweza kufanya ukuaji huu uendelee.
Back
Top Bottom