SI KWELI Malipo ya kila mwezi ya LUKU yanataka kuondolewa

SI KWELI Malipo ya kila mwezi ya LUKU yanataka kuondolewa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
TANESCO ni shirika la umeme Tanzania lenye wajibu wa kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa wananchi.

Madai

Mdau wa JamiiCheck.com amehitaji kupata ualisia iwapo ni kweli TANESCO wanakusanya namba za mita na majina ya wamiliki wakidai mapato hayo yanataka kuondolewa na kurudishwa katika halmashauri.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. JamiiCheck imewasiliana na TANESCO kupitia kwa Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Umma, Irene Stanley ambaye amekanusha kuhusu suala hilo na kuwataka wananchi kuwa makini kwa kutokutoa Taarifa.

"Hiyo taarifa haina ukweli wowote, ni uongo, Wananchi wawe makini wasitoe taarifa zozote za LUKU kwani TANESCO tunao mfumo unaomtambua mtumiaji moja kwa moja." - Irene Stanley
Back
Top Bottom