SI KWELI Lamine Yamal mwenye miaka 17 ana mtoto wa miaka mitatu

SI KWELI Lamine Yamal mwenye miaka 17 ana mtoto wa miaka mitatu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Lamine Yamal ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Hispania mwenye asili ya Morocco na Guinea Equatorial. Alizaliwa tarehe 13 Julai 2007. Yeye ni kijana mdogo ambaye ameonyesha vipaji vya hali ya juu na anaichezea klabu ya Barcelona katika ligi kuu ya Hispania, La Liga.

Picha ya Mchezaji kinda Lamine Yamal (17) akiwa amebeba mtoto (3) ikisambaa na kudaiwa kuwa ni mtoto wake imetumiwa kwenye mitandao mbalimbali tazama hapa na hapa

1721065920825-png.3043317

Moja wapo ya taarifa zinazosambaa kuhusu Lamine Yamal na mtoto aliyembeba

Ufuatiliaji wa JamiiCheck katika vyanzo mbalimbali umebaini kuwa taarifa inayodai mtoto huyo ni wa Yamal haina ukweli. JamiiCheck imebaini mtoto huyo aliyebebwa anaitwa Keyne Yamal ambaye ni mdogo wa Lamine na sio mtoto wake kama inavyodaiwa.

1721065582384-png.3043308

Taarifa inayoeleza uhusiano wa Lamine Yamal na Keyne Yamal

Endelea kutembelea Jukwaa la JamiiCheck ili kuwa karibu na taarifa zilizohakikiwa
Back
Top Bottom