Tuendeleeni tu Kuruhusu 'Upuuzi' na 'Uhuni' huu wa maneno yanayoashiria 'Ufirauni' kutumika na Makampuni ya Simu huku Serikali mkipokea Kodi yenu Kubwa na Maadili kwa Jamii na Kizazi kuzidi 'Kudidimia' tu.
Kuna Kampuni nyingine nayo nimedokezwa inataka kuja na 'Promo' yake isemayo ' Ukitaka...
TCRA na "106# wanafaidika na nini? Maana ni kama usanii.
Hiyo ni namba tuliyoambiwa kuitumia kuhakiki iwapo vitambulisho vyetu vimesajili namba ambazo hatuzitambui.
Kwa bahati mbaya kila nikijaribu wala sipati majibu. Sasa nauliza, iwapo TCRA wanatumia nguvu nyingi kuitangaza kupitia clouds...
Hiki kipindi kimekuwa kinaleta ukakasi sana katika afya ya habari nchini. Mara nyingi kimetumika kama dekio la kusafisha watuhumiwa hasa watendaji wa serikali. Kipindi kimekuwa kinaendeshwa kwa waandaji kujipendekeza rejea zama za utawala wa JPM.
MCT na TCRA chukue hatua juu ya kipindi hiki...
TCRA hivi awa matapeli kutumia simu mbona bado wapo wengí na sasa wanazidi kuongezeka si line tunasajiri na alama za vidole iweje waendelee kuwepo.
Leo naona tuanze kuolozesha humu namba za matapeli wanautuma msg zile za waganga na mtoto wako kaumia tupo hospital na wale wanajifanya huduma kwa...
Nitangulize samahani kwa wadau watakaodhani natetea uhalifu (ubaya) wa namna yoyote. Lakini wema na ubaya havijawai kuachana kama mwanga na giza. Ifikie hatua waibiwaji tujitathmini.
Ubaya ukikwaza wengi mtu timamu huangalia wapi tatizo linaanzia.
Hili la wizi wa mtandaon kama "tafadhari...
Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano latoa ushauri kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ikiwemo kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya kujiletea maendeleo
Kwenu TCRA na waziri wa mawasiliano na uchukuzi, mbona mambo hayako kama ambavyo mlitaka tuamini kuwa yatakuwa?
1. Gharama ya bundle bado zinatofautiana kutoka mtandao mmoja na mwingine japo mlisema mnaweka uniformity (Sera ya Ujamaa na Kujitegemea)
2. Hakuna kushea bando kama ambavyo...
Hongera Mh. Kalemani kwa kuwawajibisha watumishi ambao aidha wamehisika kusababisha usumbufu au vyovyote vile.
Pia Mh. Kalemani amekua muungwana kwa kuwaomba radhi Watanzania kwa usumbufu uliojitokeza.
Wakati huohuo waziri mkuu ameenda mbali zaidi kwa kutoa maagizo kwamba wakae pembeni wapishe...
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewakaribisha Watanzania, kutoa maoni yao juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki kwa matumizi.
Wito huo umetolewa leo Jumanne tarehe 11 Mei 2021, Mkoani Morgoro na Mkuu wa Sheria wa TCRA, Dk. Phillip Filikunjombe...
Mwaka jana (2020) mwezi wa kwanza TCRA ilitoa wito ya watu wote kutumia .co.tz na ukitumia .com ni kosa ambalo unaweza kulipishwa faili au kifungo.
Swali langu ni je, mpaka sasa sheria hiyo ipo? na kama bado ipo kwa nini baadhi ya watu wanaendelea kutumia .com? naomba ufafanuzi kwa wanaofahamu...
Vikundi vya haki za binadamu nchini Zimbabwe vinasema serikali imekuwa ikikiuka haki za kimsingi za watu tangu kuanza kwa ugonjwa wa COVID-19. Vikundi hivyo viliwasilisha uchunguzi wao katika mkutano wa njia ya mtandao na maafisa katika mji mkuu Alhamisi.
Katika mkutano huo, vikundi vya haki...
“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuwajulisha kwamba sasa vifurushi vya mawasiliano ya simu vimerudi kama awali, endapo kuna Mwananchi bado anapata changamoto ya huduma hii tuandikie TCRA
====
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaarifu kuwa vifushi vya mawasiliano...
Hivi ni kwanini wenye Mamlaka wengi nchini Tanzania neno Samahani ( Naomba Radhi ) Kwenu huwa ni Gumu sana huku mkidhani mkisema itakuwa mnajidhalilisha au kuonekana dhaifu?
Yaani kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka Jana ( 2020 ) hadi hii Leo Huduma ya Mtandao wa Twitter ilikuwa haipatikani mpaka...
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la kampuni za simu nchini kuwatumia mawakala kusajili laini za simu mitaani.
Akizungumza Jumatano Aprili 14, 2021 mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Jabir Bakari amesema mamlaka hiyo imeondoa zuio hilo na sasa kampuni za simu zitaendelea...
Kila kukicha tu 'Maajabu' mengi yanagundulika nchini Tanzania na huenda nchi yetu ikawa imebarikiwa Kimaajabu hadi Raia wake ni wa ajabu.
Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Makampuni ya Simu yanaweza Kupandisha bei za 'Vifurushi' haraka, ila katika Kuvishusha wanachelewa.
TCRA hongereni...
TCRA, nawaomba muichunguze kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom kwa kukata fedha unaponunua muda wa maongezi kwa hoja kuwa mteja uliomba/ulijiunga na huduma fulani ambayo hutakiwa kulipia kwa kukatwa fedha mara tu unaponunua muda wa maongezi.
Mimi binafai ni mhanga wa hili jambo kwani...
Poleni na majukumu ndugu zangu wana jamvi.
(a)Kwanini kusiwe na namba ya huduma ya TCRA?
[emoji117] Yaani mteja wa mtandao husika anaponunua kifurushi kikaisha kabla ya muda wake apige simu TCRA ili wahoji au kuchunguza uhalali wa matumizi. Hapa ikibainika mtandao umefanya wizi umrudishie mteja...
Lilitoka Tangazo TCRA kuwa warudishe vifurushi vya zamani wakati wanapitia upya new rates. Wamegoma kwa viburi na DG hajafanya lolote.
Jana Rais kampa angalizo juu ya "uchafu" uliopo TCRA. Naona bado DG amelala, haamini kama kuna uchafu katika makampuni ya simu! Wana viburi.
Au ndo haifai kuongea wakati wa kula? Au ndo wenzetu wanayumia wifi za office hawajapata taarifa? Nani wa kupaza sauti kueleza hali hii?
Kwanini mitandao mingi imekaidi?
Wanabodi mnakumbuka mwezi wa pili walipandisha bei za vifurushi, tukalalamika zipunguzwe wakatuahidi mwezi wa 4. Mwezi wa 4 vimepanda zaidi tumepiga kelele wameturudisha kwenye bei zilezile za mwezi wa pili tulizokuwa tunazipigia kelele, nasi bila kujua tunashangilia.
Kifupi Serikali...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.