Wadau, mna maoni gani kuhusu vurugu inayofanyika Afrika Kusini?

Zuma ni kiongozi fulani hivi mwenye haiba ya kuwakomboa kifikra waafrica.

Kuwakomboa waafrika kifikra? Si kweli. Ni maarufu kwa siasa za kusaka umaarufu: populism.

Huyu anafuata nyayo za viongozi wa kiafrika walioleta utawala mbovu kwenye nchi zao mara baada ya kupata uhuru. Kushika madaraka tu akaaisi ufisadi mkubwa akisaidiwa na familia ya Gupta. Wafaransa wakamvamia na miradi ya vifaa vya ulinzi wa anga na usafiri wa ndege. Familia yake ikaanza kushika hisa nzito kwenye mashirika ya umma yaliyobinafsishwa, n.k.

Kwa kifupi, ANC, chini ya kina Zuma inatajirisha viongozi weusi huku waafrika wanyonge wanazidi kuwa masikini.
 

Hakuna cha kushangaa. Weusi wengi bado masikini sana hata elimu hawana. Kufungwa kwa Zuma ni kisingizio tu cha kuhalalisha hujuma/wizi.

Viongozi wao wa ANC wanajitajirisha na fursa za kifisadi na kuwadanganya ndugu zao wanyonge kuwa adui zao bado ni makaburu na wageni toka nchi zingine za kiafrika!

It’s a hopeless situation for the blacks.
 
Maneno yako haya hayana ushahidi wowote, bali yamejaa conspiracies na uongo wa hali ya juu.
 
Serikali ikomae tu, hatutaki mambo ya mungu mtu, kama una hatia ufungwe hata kama wewe nani.
Weusi tunatia huruma sana....

Waafrika hatujazoea kuona mzito kama Zuma anaenda lupango.

Usishangae kusikia nchi nyingi za kiafrika chini ya AU zikionyesha kutoridhika na hatua hiyo.
 
Waafrika hatujazoea kuona mzito kama Zuma anaenda lupango.

Usishangae kusikia nchi nyingi za kiafrika chini ya AU zikionyesha kutoridhika na hatua hiyo.
Zuma alikuwa mwizi. Wacha afungwe tu
 
Maneno yako haya hayana ushahidi wowote, bali yamejaa conspiracies na uongo wa hali ya juu.

Soma na fuatilia mijadala na mienendo rasmi ya mambo yanayoendelea Afrika ya Kusini.

Fuatilia mwenendo mzima wa “state capture”. Na AU tayari imeanza kufanya monitoring ya masuala ya RSA kupitia mpango wake wa “early warning systems”.

Uongo wa hali ya juu? All is transparent. Tandaza hizo conspiracies hapa.
 
Mzee shutuma zisizo na ushahidi ni uzandiki. Hivi unamjua Zuma wewe!?

Hebu achana na hisia na kipuuzi kwa mtu usiyemjua.
 
Waafrika wengi wako hivyo yaani tukio ni tofauti na wanachoamua kufanya

Sio njaa bali ni ujinga wa hali ya juu kuchoma mali za watu wakati ni serikali ndio imemuwajibisha

Kuvunja maduka na kuiba, kuchoma magari ni kuzidi kudidimiza uchumi wao tu mafala hao
 
Mzee shutuma zisizo na ushahidi ni uzandiki. Hivi unamjua Zuma wewe!?

Hebu achana na hisia na kipuuzi kwa mtu usiyemjua.
Zuma ni corrupt stupid populist ambaye ameharibu uchumi wa Afrika Kusini. Ukweli haubadiliki.
 
Wafuasi wake ni wajinga. Ndio maana wanampenda licha ya yeye kuharibu uchumi wa SA.
Duh!!! Yani kitendo chako tu hiki cha kuwaita waafrika wenzako wajinga tayari kinaonesha ubinafsi wako. Don't ever call other stupid while you don't know the details.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…