Kenya 2022 Martha Karua ateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga

Kenya 2022 General Election
So kamuiga Rafiki yake JPM kumteua Samia, ndio kusema kwamba naye Raila hata maliza miaka yake ya utawala?
Hii ni fikira ya upuzi sana. Hapa Kenya wagombea wengi wamewai chagua wanawake kama wagombea wenza ila hawakushinda. Na pia wanawake wengi wamewai gombea urais akiwemo huyo huyo Martha Karua ila hawakufanikiwa. Yani Mtanzania akikuona ukipumua atasema eti umemuiga. 🤣 🤣
 
Wakenya nao siku hizi wanachezewa tu,
Huyu odinga hii ni mara ya ngapi?
Halafu hivi kenya hakuna wanasiasa waislamu?
Mbona wamepoa sanaaa
 

Martha Karua atafanya yaliyotokea TZ kwa JPM​

 
Nilikua kwenye delegation ya mkapa tulitumwa na JK... namkumbuka sana huyo mama.
Wakati huo hali ilikuwa mbaya sana. Ningependa ueleze hata kwa paragraph mbili au tatu unakumbuka nini katika hio safari yako ya Kenya. Najua hali ilikuwa ngumu ila ningependa kupata taswira kutoka kwako na kumbukumbu zako wa wakati huo.
 
Wakenya nao siku hizi wanachezewa tu,
Huyu odinga hii ni mara ya ngapi?
Halafu hivi kenya hakuna wanasiasa waislamu?
Mbona wamepoa sanaaa
Wapo wengi tu kina Joho, Aden Duale, Ukur Yattany, Junet Muhammed n.k ila kule Hakunaga siasa za kidini ndio maana Odinga licha ya kuwa mkristo anapigiwa kura miaka yote na jamii ya wapwani na wasomali ambao ni waislam 90%
 
Martha ni msafi..... Odinga kazaliwa familia ya bilionea so kakuta Hela zipo ila Ruto + Gachagua wamekulia maisha magumu Hela wamezipata baada ya kuwa viongozi wa kisiasa!!

Karua ni msafi Kenya nzima inajua Hilo, hajawahi kuwa na skendo ya wizi.
Africa hakuna huo ujinga unaousema? Hizo hela za Odinga na za kina Martha zote ni wizi tu wa mali za umma....... Africa hakuna huo ujinga unaousema
 
Wakati huo hali ilikuwa mbaya sana. Ningependa ueleze hata kwa paragraph mbili au tatu unakumbuka nini katika hio safari yako ya Kenya. Najua hali ilikuwa ngumu ila ningependa kupata taswira kutoka kwako na kumbukumbu zako wa wakati huo.
Ni kwamba Mwai alimlazimisha kivuitu kutangaza matokeo ya kughushi hali iliyopelekea Kivuitu kukimbia nchi huku nyuma akiacha fujo Kenya.

Tanzania ilikua miongoni mwa wasuluhishi wa mgogoro ule uliogharimu maisha mengi sana ya watu. Kutoka Tanzania alitumwa Mkapa na tulimsindikiza maafisa wa MFA akiwa na marehemu Koffi Annan basi bwana huyo mama akiwa waziri na mtu wa karibu na Kibaki ndiye alichochea sana machafuko Kenya kwa kiburi chake cha kukataa suluhu alifikia hatua ya kumtukana Mkapa matusi ya nguoni kwa kile alichodai kuingilia mambo yasiyowahusu.

Nilijaribu kufwatilia background ya huyu mama nikagundua hata kwa Moi walikwaruzana sana na mwanamke asiye na tone la adabu linapokuja swala la mapambano.

She is so aggressive.
 
Naona kweli ulikuja Kenya. Ni kweli Karua akichukua msimamo habanduki hata kwa mtutu wa bunduki. Ila siasa ndio hivyo, Odinga na huyu Karua sasa ni marafiki na siasa haina uadui wa milele ina uadui wa muda mfupi tu. Ila pole kusikia kwamba Karua kamtukana Mkapa. Mkapa alikuwa mzee mzuri.
 
Ndipo nami nimeamini siasa haina adui wa kudumu maana huyu Martha alitia doa sana ndoto ya Raila.....
 
Mkuu vipi huko Kenya between Raila na Ruto who is leading the race?

I wish Raila ashinde nione nini ataifanyia nchi yake, kapambana kwa miaka mingi sana.
 
Wapo wengi tu kina Joho, Aden Duale, Ukur Yattany, Junet Muhammed n.k ila kule Hakunaga siasa za kidini ndio maana Odinga licha ya kuwa mkristo anapigiwa kura miaka yote na jamii ya wapwani na wasomali ambao ni waislam 90%
Oooh ok,
Lakini kama hakuna siasa za kidini basi wangetawala wote dini hii na dini hii,
Lakini dini moja tu inatawala miaka yote huo sio udini?
Hapa nazungumzia nafasi tatu za juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…