Maandamano Kenya sasa mara 2 kwa wiki

Yawezekana unajua Siasa ya Kenya vizuri it's okay but Ruto kashinda state ww!
State ipi? Mind you Uhuru is supporting Odinga so it's not like he's alone, ana back up ya richest man in Kenya. Kingine Odinga akiuwawa ndio itakua mwisho wa nchi kutawalika.

The only option is either handshake au ajiuzulu otherwise itakua nchi ya maandamano na migomo, baadae utasikia Al Shabaab wamevamia airport n.k

Ruto is not smart, otherwise he would've seen this coming.
 
The only option is either handshake au ajiuzulu otherwise itakua nchi ya maandamano na migomo, baadae utasikia Al Shabaab wamevamia airport n.k

Ruto is not smart, otherwise he would've seen this coming
Hicho ndicho anachokitaka Mzee Raila, hizo sababu nyingine zinatumika tu kama 'cover' ya kufanikisha hilo.
 
Alie turoga africa kafa.. na hao wa andamanao machizi... Yaani mtu hata mwaka hauja kamilika Wanaanza kulaumu? Yaani Hapo mijitu imepewa vibakuli vya Gidheri na sukuma wiki.... KWa upuuzi wao imeingia road.... Shame on them... Wanasiasa wanawatumia KWa faida zao binafsi....
 
Raila anataka cheo, wagawane position waone kama atapiga kelele!! Anajidai kutetea wananchi kumbe matumbo yao
 
Hana lolote zaidi ya maslahi binafsi.
Before nilikua namuunga mkono sana huyu mzee, ila nimetafakari sana hizi movements zake nmeona anawatumia wafuasi wake kama tool ya kumtengenezea nafasi kwenye serikali. Ilikua hivyo 2007 kwa Kibaki, alipoukwaa u PM akapoa.
2017 akaibuka tena baada ya kushindwa uchaguzi, akaleta maandamano ya kila jumatatu hadi akajiapisha kuwa rais wa watu, Kenyatta akanywea akamkaribisha kwenye shake hand,, wakatengeneza BBI, kisha waje wabadilishe katiba ambayo huyu Raila alishiriki kuiunda 2010. Timu Ruto ikaenda courtini BBI ikatupwa kwa amri ya mahakama. Uhuru alimuunga mkono kwa uchaguzi uliofuata wakapigwa na Ruto ambaye hata huo urais wa Uhuru yeye ndiye ali-uinjinia.
Leo analeta yaleyale yaliyosababisha kuwe na shake hand 2018. Binafsi siungi mkono madai yake mawili due to these 2 facts
1. Hali ngumu ya maisha haijaletwa na serikali ya Ruto iliyoingia miez michache iliyopita. Hata hiyo serikali imeikuta hali ngumu. Kumbukeni jinsi wakat wa kampen za uchaguzi wao kulivyotawaliwa na sakata la kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa zingine ikiwemo unga wa mahindi. Hivyo kwa maoni yangu sioni kama ni sawa kuilaumu serikali ya Ruto kwa ajili ya kupanda kwa gharama za maisha. And ofcourse garama zimepanda koote tu. Au anaweza kusema ni nini exactly serikali imekifanya kupelekea kupanda huko kwa gharama? And mbona hasemi what sekali should do kuondoa hilo tatizo? Anatumia hilo neno ili kuwachonganisha watu wa chini na serikali, waone kuwa kumbe ugumu wa maisha wa sasa umeletwa na serikali ya Ruto of which sio kweli. Hata wakat wa Swahiba wake Uhuru ugumu ulikuwepo pia. Ni kama ilivyokuwa 2018, maandamano yake yalikoma baada ya yeye kufanya shake hand na Kenyata, jiulize yale yaliyomfanya aandamane wakat ule yalitatuliwa baada ya yeye kupeana mikono na rais??? Jibu ni hapana ila alisitisha maandamano baada ya lengo lake binafsi kutimia.
2. Anasema serikali haikushinda kihalali. Lakini ni yeye aliyefungua kesi kwenye mahakama ya upeo kupinga ushindi wa Ruto akiwa na madai kadhaa. Na tuliona jinsi alivyopeleka vielelezo vya ushahidi wake kwa gari lakini mahakama ilitupa madai yake ikisema hakukua na ushahidi. Sasa anawaambia watu wamuamini kuwa uchaguzi uliibiwa ingali alishindwa kuthibitisha madai hayo kwenye mahakama. Poor him,,, simuungi mkono tena. Anawatumia raia maskini na umaskin wao kama daraja la kuketi meza moja na watawala. Bahati mbaya amekutana na mafia mwenye kiburi Ruto ambaye hatishiki kirahisi kama Kenyatta... let's wait and see but I hope REGGAE will stop kama ilivyostopishwa REGGAE ya BBI.
 
Kinachowauma common people ni hali zao kuwa ngumuuuu huku viongozi wao wakijichotea mahela kibao ya posho,mishahara nk
 
Olengurumwa aione hii kwenye shajara
 
Mnachokitaka mtakipata. Yote kwa sababu kuna mtu anayeamini kuwa kiti cha urais ni chake.

Amandla...

Kenya huo ni Muziki mwingine. Tuone aibu kuwashauri hao. Kwetu Iko wapi katiba mpya kama kipaumbele?

Sana sana:

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

8. Raila au wakenya katika Mapambano si wajinga wanayo hoja na wanakijua wanachokipigania.

#8 hiyo inawahusu zaidi aliowaangazia Dkt. Mollel:

 
Hii maandamano ya Kenya isipokoma kunaweza zuka majanga watayojutia wote mbeleni
 
Kashindwa kwenye sanduku la kura sasa anatafuta njia nyingine....

Kudhani nyomi yote ile ni wapuuzi, ila sisi kwa hakika itakuwa trespassing.



8. Raila au wakenya katika Mapambano si wajinga wanayo hoja na wanakijua wanachokipigania.


Hawawezi kuwa wajinga watu hao wote eti kuwa ila sisi.

Ndiyo maana bila katiba mpya kwa mara nyingine tunaanza kupanga uchaguzi tena tukikenua:

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?
 
Mkuu wakenya wanayajua matatizo yao na suluhu zao vyema zaidi kuliko mtu yeyote aliye hai duniani.

8. Raila au wakenya katika Mapambano si wajinga wanayo hoja na wanakijua wanachokipigania.

Kudhania watu wote hawa ni wajinga ila sisi?



Huko itakuwa ni kujilisha upepo bure ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…