safi sana mkuu hapo juu, pia huwa nawadha, hivi kuke mitaa ya singida kule ambapo ndio nimekulia, kule huwa tunahitaji hela ya kwenda kusagia tu debe la ,mahindi au mtama, na mafuta ya taa kwa ajili ya koboroi tena unawasha wakati wa kutandika tu au kama kuna mwanafunzi anapigia book, LOL, maana msosi upo, mboga ipo, maana mifugo kibao maziwa nakadhalika, shopping labda mpka siku ya mnada au gulio, sasa kwa watu wanaojitosheleza hivi, na statistics za spending zao ni vigumu kupata ila hawa watu sio masikini, watu hawa huwa wanakua clasified vipi? maana nimetolea mfano kieneo kimoja , maeneo mengi TZ bado ni vijiji na hizi statistics za spending , CPI, sijui hata wanapimaje,