Mwanahabari wa kampuni ya MediaMax inayomiliki K24 na Milele FM, Catherine Wanjeri Kariuki, ameruhusiwa kuondoka hospitali leo baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye mguu wake uliopigwa risasi kwenye maandamano ya #RutoMustGo jijini Nakuru.
Catherine ambaye alikuwa kazini akiripoti mubashara kuhusu maandamano aliopigwa risasi mbili kwenye mguu wake wa kushoto.